Ili jukwaa letu liwe mahali pazuri kwa kila mwanachuo, tafadhali fuata kanuni hizi.
Heshimu maoni, mitazamo na maoni ya wanachuo wenzako. Hakuna matusi, kebehi, au unyanyasaji wa aina yoyote.
Tumia Kiswahili au Kiingereza. Epuka maneno machafu, kejeli, au lugha ya chuki kwa mtu, kikundi, au taasisi.
Chagua kategoria inayofaa kwa thread yako. Hii inasaidia wengine kupata mijadala kwa urahisi.
Usirudie kuchapisha mada hiyo hiyo. Usitumie jukwaa kwa matangazo ya bidhaa au huduma bila ruhusa.
Hakuna maudhui ya ngono, ukatili, pombe, au madawa ya kulevya. Hakuna kushiriki habari za uongo au kudanganya.
Usishiriki taarifa za kibinafsi za mtu mwingine bila ruhusa. Hii inajumuisha picha, namba za simu, na emails.
Kutishia, kudhulumu, au kuhujumu mtu yeyote — iwe kwa maneno au vitendo — ni kosa kubwa.
Kanuni zote za nchi yetu zinatumika kwenye jukwaa letu. Hakuna kuvunja sheria kwa njia yoyote.
Ukiukaji wa kanuni unaweza kusababisha onyo, kuondolewa kwa maudhui, kufungiwa akaunti kwa muda, au kufutwa kabisa kwa akaunti yako — kulingana na uzito wa kosa.
Una swali kuhusu kanuni? Wasiliana nasi kwa hello@mwanachuoforums.com