Rudi
@mwanachuo_forumsVerified account · 1 day
Mdahalo Pinned

Karibu Mwanachuo Forums — Sauti Yetu, Safari Yetu

Kuna wakati mmoja nilikuwa chuoni, nimekaa kwenye kimbweta jioni. Nilikuwa na maswali mengi kichwani — kuhusu ajira, kuhusu maisha baada ya chuo, kuhusu ndoto zangu. Nilijisikia mpweke. Kila mtu alionekana ana jibu lake binafsi, lakini mimi nilikuwa na maswali tu.

Sikuwahi kujua wa kumwambia. Sikuwahi kujua wa kumuuliza.

Siku hiyo nilijiapiza kitu: siku moja nitatengeneza mahali ambapo hakuna mwanachuo atakayejisikia mpweke tena. Mahali ambapo kila swali lina jibu, kila wazo lina mtu wa kulijadili, na kila ndoto ina mtu wa kuisupport.

Leo, hapa tulipo. Mwanachuo Forums ni ndoto ile iliyokomaa.

Hii ni nyumbani kwako.
Hapa, kila mwanachuo ana sauti. Kuanzia CBE hadi IFM, UDSM hadi UDOM, kuanzia Mzumbe hadi SUA, kuanzia vyuo vya kati hadi vyuo vikuu vya kimataifa — hakuna chuo kikubwa, hakuna chuo kidogo. Sisi ni wanachuo. Tuna jambo moja linalotuunganisha: safari hii tunapita wote pamoja.

Hapa tunaweza kujadili:
- Ajira baada ya chuo — ukweli, changamoto, na fursa
- Maisha ya chuo — hostel, pesa, mahusiano, stress, furaha
- Scholarship na fursa za kimataifa
- Habari za vyuo vyetu na mabadiliko yanayokuja
- Mtaa na jamii — kwa sababu chuo si kisiwa
- Ujasiriamali, teknolojia, na mawazo mapya
- Na kila kitu kinachokugusa kama mwanachuo

Kwa nini nimeanzisha hii?
Kwa sababu naamini kila mwanachuo ana kitu cha kushare. Unaweza kuwa na jibu ambalo mwenzako analitafuta. Unaweza kuwa na swali ambalo linamfanya mwenzako afikiri. Unaweza kuwa na ndoto ambayo itawasha ndoto ya wengine.

Sisi ni kizazi cha wanachuo wa Tanzania. Hatuna muda wa kusubiri. Hatuna muda wa kusema "siku moja". Siku ni leo.

Kanuni moja tu ya hapa:
Heshimu. Heshimu mwenzako, heshimu maoni yake, heshimu safari yake. Hatuwi hapa kuhukumu — tumewe hapa kujengana.

Kwa kila mwanachuo anayesoma hii:
- Kama una swali — uliza. Hakuna swali la kijinga hapa.
- Kama una jibu — shiriki. Unaweza kuokoa mtu.
- Kama una ndoto — iweke hapa. Tutaijenga pamoja.
- Kama una hofu — iseme. Hakuna mtu atakayekuonea.
- Kama una ushindi — ushiriki. Tusherehekee pamoja.

Hii thread itabaki hapa milele. Siku moja, tutarudi hapa na kutazama nyuma. Tutakumbuka mahali tulipoanzia. Tutakumbuka ndoto ile ya kwenye kimbweta mpaka kuja kuwa kweli.
Karibu nyumbani, mwanachuo.

Safari yetu inaanza hapa. Sasa.
— MwanachuoForums
312

Maoni (6)

a
@alanmox441gmailcom · 2 hrs
uhakika saana
M
@Mercy · 1 hr
❤️❤️❤️❤️