Rudi
@mwanachuo_forumsVerified account · 2 hrs
Maisha ya Chuo

Uzoefu wangu: Jinsi nilivyopoteza Boom ndani ya wiki moja na nilivyosurvive chuo! ๐Ÿ’€๐Ÿ’€

Uzoefu wangu: Jinsi nilivyopoteza Boom ndani ya wiki moja na nilivyosurvive chuo! ๐Ÿ’€๐Ÿ’€
Inasikitisha lakini ndio ukweli. Muhula uliopita, mara baada ya meseji ya Boom kusoma kwenye simu, akili ilihama. Nilijiona Mkurugenzi!

Wiki ya kwanza nilifanya haya makosa:
โ€ข Nikanunua viatu vipya viwili (visivyo na mpango)

โ€ข Nikalipia "sub" ya Netflix ya miezi mitatu mbele

โ€ข Kila jioni nikawa mtu wa kuagiza chips kuku na washkaji

Kufika siku ya 8, naenda kuangalia salio ATM... nikakuta zimebaki Tsh 14,300 tu! Wakati huo bado miezi mitatu mbele ndio Boom lingine lije. Nilichoka! ๐Ÿ˜‚
Nilivyosurvive (Mbinu zilizoniokoa):

โ€ข Uji wa Muhogo: Nilinunua unga wa muhogo wa Tsh 3,000 na sukari robo. Ukawa ndio mlo wangu mkuu asubuhi na usiku.

โ€ข Kazi za Kuchapa (Typing): Nilikuwa na laptop chumbani. Nikaanza kuwasaidia washkaji kutyper assignment zao na kuwadesignia mawasilisho (powerpoint presentation). Kazi moja nikaliza Tsh 2,000 hadi 5,000. Hiyo ndio ilikuwa inaleta mboga.

โ€ข Kutembea kwa miguu: Niliahidi sitapanda bajaji wala pikipiki kwenda darasani. Nikawa mtu wa "route" za miguu ili kuokoa Tsh 1,000 kila siku.

Somo nililojifunza: Boom sio hela ya kutanua, ni hela ya kukusaidia ukae darasani usome. Usipoiheshimu, itakutesa!
๐Ÿ‘‰ Wewe ushawahi kufanya matumizi gani ya hovyo baada ya Boom kuingia? Shusha story yako hapa chini!
16

Maoni (0)

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza!